Serikali ya Kenya imetangaza kuchukua hatua kali zaidi za
kiusalama kwa lengo la kukabiliana na kundi la kigaidi la al Shabab la
nchini Somalia. Taarifa kutoka Nairobi zinasema kuwa, hatua hiyo ya
serikali ya Kenya imechukuliwa baada ya kushadidi mashambulio ya kundi
la al Shabab nchini humo. Aidha serikali ya Kenya imeongeza muda wa
kuwaweka rumande washukiwa wa ugaidi kutoka siku 90 hadi 360 pamoja na
kusimamia kikamilifu idara ya mawasiliano nchini humo. Mpango huo pia
umelenga kupunguza idadi ya wakimbizi wa kigeni walioko nchini humo na
kufikia laki moja na nusu, ikilinganishwa na wakimbizi laki sita na elfu
saba walioko hivi sasa kwenye kambi za wakimbizi nchini humo. Hali
kadhalika, serikali ya Kenya imetangaza kuwa, waandishi wa habari ambao
watapatwa na hatia ya kuzuia kufanyika uchunguzi na operesheni za
kupambana na ugaidi watahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela. Hali
kadhalika, waandishi wa habari watakaotumia suhula za kijamii kwa lengo
la kuwashawishi wananchi kutekeleza operesheni za kigaidi watahukumiwa
adhabu ya kifungo cha miaka ishirini jela. Inafaa kuashiria hapa kuwa,
serikali ya Kenya inakabiliwa na mashinikizo makubwa yanayotokana na
mashambulio ya kigaidi, tokea kiliposhambuliwa kituo cha kibiashara cha
Westgate jijini Nairobi mwezi Septemba mwaka jana, na kupelekea watu
wasiopungua 67 kuuawa. Mapema mwezi huu, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
aliwafuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na Mkuu wa Jeshi la
Polisi baada ya kuongezeka mashambulio ya kundi la kigaidi la al Shabab
katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo
No comments:
Post a Comment