Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora
wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana. Baada ya maelfu ya kura
kuhesabiwa, mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine Brahimi ndiye
mshindi wa mwaka huu.
Hapajawahi kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa
mchezaji bora kutoka Algeria kuishinda, lakini Brahimi amefanikiwa
kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe wa 2014.
Aliingiza bao la ushindi dhidi ya mabingwa wa Hispania Barcelona, bao
lengine la kisasa katika ligi ya mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika
msitari wa mbele wakati nchi yake iliposonga mbele katika michuano ya
kombe la dunia. Yacine Brahimi
Hio ilikuwa historia kwa Algeria kufika katika awamu ya muondoano katika dimba hilo.
Hii bila shaka ilikuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa BBC pamoja na
wapenzi wa soka kumchagua kama mchezaji bora zaidi wa Afrika mwaka huu.
Aliwapiku wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang
wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na
hatimaye Yaya Toure – aliyenyakua ushindi mwaka jana.
No comments:
Post a Comment