Kaimu
Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (mwenye suti nyeusi)
aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo, akiongea na
Vijana wanaofanya shughuli za kujitolea wakati wa maadhimisho ya siku ya
kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
juma.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya vijana kutoka taasisi mbalimbali na mashirika
yasiyo ya kiserikali waliohudhuria maadhimisho ya siku ya kujitolea
kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma
wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Waziri Mukangara iliyosomwa kwa niaba
yake na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (hayupo pichani).
Mkufunzi
wa ujasiriamali kutoka shirika lisilo la kiserikali la Restless
Development, Lawrence Ambokile, akitoa ushuhuda wake kwa vijana wenzake
ambapo alisema anajisikia faraja na moyo wake una furaha kwa kufanya
kazi za kujitolea kwenye jamii ambapo imemsaidia kukuza uelewa wake na
pia ni baraka kwa Mungu.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui akifafanua
jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma yaliyokutanisha vijana kutoka
taasisi na mashirika mbalimbali yasiyoyakiserikali wanaofanya shughuli
za kujitolea kwenye jamii.
Vijana
wanaofanya shughuli za kujitolea kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa
wamekusanyika pamoja kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
kujitolea yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi (kulia) akiwa
ameongozana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt.
Steven Kisui, Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC), Stella Vuzo aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja
wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakielekea kutembelea mabanda kwenye
maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa juma.
Mfanyakazi
wa Shirika la KOICA, Catherine Tarimo akieleza shughuli mbalimbali
wanazofanya ikiwemo kujitolea kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo
ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James
Kajugusi (mwenye suti nyeusi) aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana ya
wizara hiyo. Kushoto kwake ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo na kulia kwake ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui.
Mwakilishi
wa kampuni ya 4Life, Nelson Benges (mwenye tai ya damu ya mzee)
akielezea virutubisho mbalimbali vinavyotumika kuimarisha kinga ya mwili
wa mwanadamu kwa asilimia 437 na kuufanya mwili imara na uweze kupamba
na magonjwa kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi Kulia
kwa Bw. Kajugusi ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo na kushoto kwake ni Programme Officer wa
Shirika la UNV, Bi. Stella Karegyesa.
Mtaalam
wa Masoko wa UN Volunteer Kitaifa, Catherine Sinje (wa pili kulia)
akieleza shughuli mbalimbali za kujitolea zinazofanywa na shirika lake
likiwahusisha vijana zaidi katika kufanya kazi za kujitolea kwenye jamii
kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi wakati wa
kutembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Kaimu
Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi, akizungumza jambo na
wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) alipokuwa
akitembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Na Mwandishi wetu
SERlKALI imesema inatoa kipaumbele kwenye suala la kujitolea ikiwa ni sehemu ya kushirikisha vijana katika maendeleo yao na taifa lao.
Kauli hiyo
imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya
vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,James Kajugusi
wakati akisoma hotuba kwenye madhimisho ya Siku ya Kimataifa yakujitolea
kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Fenela Mkangara.
“ Kama nchi
serikali inadhani kujitolea ni hiari si kitu cha kulazimisha… unafanya
kwa hiari bila kusukumwa na mtu au kitu inajenga nidhamu.Serikali
inaamini kujitolea ni utu na unaonesha ubinadamu wako kwako wewe
mwenyewe kwa watu wengine na kwa nchi yako.”
Kaimu
Mkurugenzi huyo alisema kwamba kutokana na Serikali kuthamini na
kutambua mchango wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya nchi ,ambapo
washiriki wake wengi ni vijana, inapanga mkakati wa kutumia uzoefu wa
vijana hao katika masuala hayo ili kuinua ushiriki wa vijana katika
maendeleo ya nchi.
Alisema
ingawa kujitolea kunawezesha kupata uzoezi ili vijana waweze kuajiriwa
na kuendeleza taaluma,maana ya kujitolea haipo katika kuajiriwa bali
katika hali ya kuona maana yake katika kusaidia jamii kujitambua na
kujituma na kuwajibika .
“Usaidizi
katika jamii ndio muhimu kuliko ajira. Haina maana yoyote kuwa na ajira
bila kujua maana yake katika kusaidiajamii,” huku akisisitiza kwamba
haina maana yoyote kama umeajiriwa na ukaendekeza umimi huku ukiwa
hujali maslahi ya umma hata yanapoharibika.
Alisema
Serikali ikiwa inaamini kwamba chachu ya kujitolea ni vijana ametaka
watumie njia mbalimbali katika shughuli za kujitolea kwa kuona wenzetu
wanafanya nini na kutumia uzoefu wao katika kujenga taifa imara la
Tanzania.
Aidha alisema
wakati umefika wa vijana kusaidia kurejesha moyo wa kujitolea
uliokuwepo kabla ya miaka ya 1970 ambapo shughuli za maendeleo ikiwemo
ujenzi wa barabara ulifanywa na wananchi wenyewe kwa namna ya kujitolea
kuanzia miaka ya 1970 moyo wa kujitolea umepungua sana.
“Nilikozaliwa
wananchi ndio walikuwa wanatengeneza barabara, visima vya maji,
wananchi ndio wanapeleka wagonjwa hospitali..’” na kusema kwamba sasa
hali imekuwa mbaya kwa kuwa inadaiwa kitu kwanza kabla ya kufanyika kwa
kazi.
Akizungumzia
kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kujitolea inayosema; Ushiriki na
ushirikishwaji katika kuleta maendeleo katika ngazi zote za kitaifa na
za kimataifa, amesema inaangalia ushiriki wa vijana katika maendeleo.
Alisema
Tanzania imetengeneza mikakati kadha aya kuwezesha ushiriki wa vijana
ikiwa ni pamoja na kuridhia mkataba wa vijana wa umoja wa Mataifa na
kuanzisha baraza la vijana kwa mujibu wa katiba.
Naye Afisa
habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo
akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini, Alvaro Rodrigues, amesema umoja wa mataifa unajisikia faraja
kuadhimisha siku hiyo ikiwakumbuka watu mbalimbali waliofanya utu kwa
kujitolea katika shughuli mbalimbali za ubinadamu.
Akiwasilisha
neno la katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki moon alisema siku ya
kimataifa ya kujitolea ni muhimu kutokana na mahitaji halisi yaliyopo
sasa duniani katika ulinzi wa maisha ya binadamu na utamaduni wake.
Alisema
maelfu ya wananchi waliokumbwa na madhila mbalimbali wameweza kutulizwa
na wafanyakazi wa kujitolea ambao waliondoa umimi na ubinafsi na
kusaidia walio katika matatizo.
Alisema Umoja
wa mataifa ukiwa unathamini amani , haki sawa na maendeleo ya jamii na
kwa kuwa na siku ya kujitolea ya kimataifa kunaonesha umuhimu wa juhudi
za umoja huo za kusambaza malengo hayo kufanikisha maendeleo na ushiriki
wa vijana katika maendeleo yao , kitaifa na kimataifa.
Katika hotuba
yake ya kumkaribisha mgeni rasmi, Vuzo alisema kwamba shughuli za
kujitolea za Umoja wa Mataifa zilianza nchini mwaka 1974 katika misingi
ile ile ya kufunza jamii kujitolea kwa manufaa yao na maendeleo ya
taifa.
Vuzo alisema
programu ya kujitolea ya Umoja wa mataifa ambayo hapa nchini inaitwa UNV
inasaidia kufanikisha mikakati mbalimbali inayoendeshwa na serikali ili
kuboresha hali ya kujitolea nchini kwa manufaa ya taifa.
Programu hiyo
ikiwa imezingwa na mikakati ya kitaifa ya kukabiliana na umaskini kama
MKUKUTA na MKUZA na misaada kwa mipango ya maendeleo ya Umoja wa mataifa
UN kuanzia mwaka 2011 – 2016, UNV kwa sasa inajishughulisha na masuala
ya wakimbizi, utawala bora, Ukimwi vijana na maendeleo sekta binafsi.
Alisema UNV
ikiwa imetimiza miaka 35 imekuwa ikiwasaidia Watanzania katika sekta
hizo ambapo wamekuwa wakifanya kazi kwa moyo mmoja kuhakikisha maisha ya
watanzania yanabadilika.
Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na shughuli za kujitolea kutokana na umuhimu wake kwao na kwa taifa.
No comments:
Post a Comment