Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Friday, 12 December 2014

Jonathan kuchuana na Buhari uchaguzi wa rais Nigeria

Uchaguzi wa urais nchini Nigeria unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na wa aina yake baada ya vyama vikuu kuwachagua wagombea wao. Chama tawala cha PDP kimemteua Rais Goodluck Jonathan kuwa mgombea wake huku muungano mkuu wa upinzani wa APC ukimteua rais wa zamani, Jenerali Mohammadu Buhari kupeperusha bendera yake kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 15 mwakani. Buhari amemshinda mpinzani wake wa karibu, Atiku Abubakar, ambaye ni makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi wa ndani wa APC uliofanyika hapo jana.
Kampeni za uchaguzi zinatarajiwa kuwa ngumu hasa kwa upande wa chama tawala kutokana na serikali kuonekana kushindwa kudhibiti kundi la kigaidi la Boko Haram. Pia serikali ya Rais Jonathan itakuwa na kibarua kigumu kuwashawishi wapiga kura kwani inatuhumiwa kuhusika na ufisadi. Wajuzi wa mambo wanasema Jenerali Buhari ana sifa nzuri ya kupambana na ufisadi kwani alipoingia madarakani 1983 kupitia mapinduzi ya kijeshi alichukua hatua muhimu kukabiliana na uozo huo kabla ya kuondolewa madarakani 1985 kwenye mapinduzi mengine ya kijeshi yaliyoongozwa na Ibrahim Babangida

No comments:

Post a Comment