Shirika la kutetea haki za binadamu la Syrian Observatory for
Human Rights limesema kuwa magaidi wa Syria wamewaua raia wasiopungua
311 kati ya mwezi Julai na Disemba mwaka huu katika mkoa wa Aleppo
ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Shirika hilo limesema kwenye ripoti yake mpya kuwa, wanawake 25 na watoto 42 ni miongoni mwa raia wasio na hatia waliouawa na magaidi hao. Ripoti hiyo inasema magaidi wamekuwa wakitumia silaha zilizopigwa marufuku kwenye vita vya Syria. Taarifa ya shirika hilo lenye makao yake mjini London, Uingereza, imelaani mauaji ya raia na kuvitaka vyombo vya kimataifa kuchunguza kadhia hiyo na kuwachukulia hatua wahusika.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, takriban watu laki mbili wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kutokana na vita nchini Syria. Mgogoro wa Syria umeshindwa kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia kutokana na uungaji mkono mkubwa wa Wamagharibi na Wazayuni kwa makundi ya kigaidi yanayopigana na serikali ya Rais Bashar Asad wa nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment