Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza
kuwa Saudi Arabia imetumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa dhidi
ya wananchi wa Yemen katika mashambulio yake ya kijeshi katika nchi hiyo
ya Kiarabu. Tamim Shami Msemaji wa Wizara ya Afya ya Yemen ameeleza
kuwa baadhi ya watu waliojeruhiwa katika mashambulizi ya Saudia wana
dalili zinazoashiria kwamba wameathiriwa na silaha ziliopigwa marufuku
zilizodondoshwa na ndege za Saudi Arabia katika mashambulizi yake katika
mji mkuu wa Yemen Sana’a yaliyoanza Machi 26 mwaka huu pasina
kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa Wizara ya Afya ya Yemen
ameongeza kuwa nchi hiyo inasumbuliwa na hali inayozidi kuwa mbaya ya
kibinadamu kutokana na kuwepo uhaba wa suhula za tiba. Amesema watu
zaidi ya 5,000 wanaugua homa ya dengue na malaria.
No comments:
Post a Comment