Saturday, 6 June 2015
'Umaanawi wa mfumo wa Kiislamu Iran ni wa kipekee'
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema mfumo wa Kiislamu
wa Iran ni wa kipekee duniani kutokana na umaanawi wake. Ayatullah
Mohammad Imami Kashani, khatibu wa muda wa sala ya Ijumaa wiki hii
Tehran ameashiria umuhimu na nafasi ya mfumo wa Kiislamu wa Iran na
tafauti yake na mifumo mingine duniani na kusema: "Sira ya kivitendo ya
Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ni yenye thamani kubwa
sana ambayo inapaswa kuzingatiwa na jamii hasa kizazi cha vijana."
Ayatullah Imami Kashani aidha ameashiria namna Imam Khomeini MA
alivyolipatia umuhimu suala la umoja wa ulimwengu wa Kiislamu na kusema:
"Umoja wa Waislamu, uchumi, maisha bora ya wananchi, na kumfahamu adui
ni kati ya nukta muhimu katika sira ya kivitendo ya Imam." Ameongeza
kuwa sira ya kivitendo ya Imam Khomeini MA haiwezi kamwe kupotoshwa.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameongeza kuwa: 'Baada ya kuaga dunia Imam
Khomeini MA, uwepo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu,
Ayatullah Khamenei, ni neema kubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu. Wilaya au
uongozi wake ni muhimu sana kwa mfumo na jamii a Kiislamu kwa sababu
anafuata ile ile njia ya Imam Khomeini MA." Ayatullah Kashani
ameashiria nafasi ya 'Faqihi Mtawala' au Wilayat Faqih katika mfumo wa
Kiislamu na kusema wale ambao wanatilia shaka utawala huo ni maadui wa
mfumo wa Kiislamu. Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijumaa sambamba na
kuelezea matumaini yake kuwa kadhia ya nyuklia itatatuliwa sambamba na
kuhifadhiwa haki za taifa la Iran, ametoa wito kwa timu ya Iran katika
mazungumzo ya nyuklia kulinda haki za taifa hili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment