Kundi la kigaidi na kitakfiri la Al-Shabab linapanga njama ya
kutekeleza mashambulizi nchini Kenya katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Hayo yamedokezwa na Inspekta Mkuu wa Polisi Kenya Joseph Boinnet.
Akizungumza jana na waandishi habari jijini Nairobi, Bw Boinnet alisema
kundi hilo la kigaidi limekuwa likipanga kutekeleza msururu wa
mashambulizi katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ila halitaweza kwani
serikali imegundua njama hiyo na usalama umeimarishwa. Ameongeza kuwa Al
Shabab wanalenga kuhujumu taasisi za kiserikali, maduka, masoko, maeneo
ya kidini, vyuo vya elimu, maafisa wa usalama na waandishi habari
wanaoandika habari dhidi ya kundi hilo la kigaidi. Afisa mkuu wa polisi
Kenya amesema, "Nawahakikishia ndugu na dada zetu Waislamu kuwa wataweza
kutekeleza ibada za Ramadhani bila kuwepo pingamizi."
Aidha Boinnet ameonya kwamba wanachama wa al-Shaabab wanatumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na WhatsApp kuwahadaa wananchi kwa kutumia akaunti fiche na blogu.
Kenya iko katika hali ya tahadhari kufuatia mauaji ya kigaidi yaliyotekelezwa mapema mwezi Aprili na Al Shabab kwenye chuo kikuu cha Garrisa ambapo watu 148 waliuwawa na zaidi ya 70 kujeruhiwa

No comments:
Post a Comment