Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema haiungi mkono rais wa
Rwanda, Paul Kagame kugombea tena muhula wa tatu kwenye uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwaka 2017. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Marekani anayehusika na masula ya Afrika amewambia waandishi wa habari
mjini Washington kuwa, Rwanda inahitaji kuwa na taasisi zenye nguvu
zitakazosimamia uimarishwaji wa demokrasia na wala haihitaji mtu mwenye
nguvu kufanya kazi hiyo.
Siku chache zilizopita, wabunge wa Rwanda walifichua kwamba,
mamilioni ya Wanyarwanda wamemuomba Rais Paul Kagame kuendelea
kuwaongoza hata baada ya 2017. Kwa msingi huo, wabunge hao wamesema
watachunguza kwa makini maombi hayo ya wananchi na iwapo yatakuwa na
uzito, wataanza mchakato wa kubadilisha katiba ili kuondoa kifungu
kinachoweka kikomo kwa muhula wa rais kuongoza. Kwa sasa katiba ya
Rwanda inasema rais anayechaguliwa hawezi kuzidisha zaidi ya mihula
miwili madarakani
No comments:
Post a Comment