Habari kutoka Ghana zinasema kuwa, idadi ya watu waliofariki
dunia kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta katika mji
mkuu Accra imepanda na kufikia 175. Duru za hospitali zinasema watu
wengi waliokimbizwa kwenye vituo vya matibabu wakiwa na majeraha mabaya
ya moto wamefariki dunia kati ya jana usiku na leo mchana. Mlipuko huo
ulitokea siku ya Jumatano wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi
katika kituo cha mafuta kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.
Tarayi Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo
hivyo. Rais John Dramani Mahama ambaye ametemelea eneo la mkasa huo
amesema taifa limetikiswa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha
kwenye mlipuko huo.
Mvua za masika zinazoendelea kunyesha huko Ghana zimesababisha nyumba
nyingi kuharibika na hivyo kuwaacha watu wengi bila makao. Wizara ya
Afya ya nchi hiyo imetahadharisha
No comments:
Post a Comment