Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Monday, 15 June 2015

Magaidi wanaorudi kutoka Syria, Iraq ni hatari Balkan'

Shirika la Ubunifu la Mediterranean limeonya juu ya hatari ya kurejea magaidi katika eneo la Balkan kutoka katika nchi za Iraq na Syria. Mtandao wa Intaneti wa al Alam umelinukuu shirika hilo likisema hayo huko Sarajevo, Mji Mkuu wa Bosnia na kuongeza kuwa, hivi sasa kuna raia 115 wa Bosnia ndani ya kundi la kigaidi la Daesh katika nchi za Iraq na Syria. Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi hiyo, eneo la Balkan linakabiliwa na hatari ya vitendo vya kigaidi kama vinavyoendelea hivi sasa huko Iraq na Syria kutokana na kurejea nyumbani raia wa nchi za eneo hilo waliopigana kwenye makundi ya kigaidi katika nchi hizo mbili za Kiarabu. Kwa mujibu wa shirika hilo, hatari hiyo inazikabili nchi zote za eneo la Balkan na hata Russia kutokana na baadhi ya raia wa nchi za Serbia, Albania, Macedonia na Montenegro kuwa na uhusiano wa karibu na makundi ya kigaidi kama vile Daesh. Takwimu za idara ya mahakama ya Bosnia zinaonesha kuwa karibu watu 192 wenye umri wa miaka 25 na vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 17 wametembelea maeneo yenye mapigano huko Iraq na Syria kuanzia mwaka 2012 hadi mwishoni mwa mwaka jana. Shirika hilo limeitaka polisi ya Bosnia kuongeza nguvu za kudhibiti mitandao ya Intaneti na ya kijamii kwani ndiyo njia kuu inayotumiwa kuwashawishi vijana hao kujiunga na makundi ya kigaidi.

No comments:

Post a Comment