Rais wa zamani wa Marekani George W.
Bush amemkosoa Rais wa nchi hiyo Barack Obama kutokana na stratijia
anayotumia katika vita dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh
(ISIL) na kusema kuwa Washington inapaswa itume wanajeshi wake nchini
Iraq. Bush amesema msimamo wake ni kwamba kuna haja ya kutuma vikosi vya
nchi kavu nchini Iraq. Bush amedai kuwa serikali yake iliushinda
mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda wakati ilipotuma askari wa ziada nchini
Iraq. Barack Obama amekuwa akilaumiwa vikali kwa kushindwa
kulisambaratisha kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika nchi za
Iraq na Syria. Mapema wiki hii Obama alikiambia kikao cha nchi tajiri
zinazounda kundi la G7 kilichofanyika nchini Ujerumani kwamba hawajawa
na stratijia iliyokamilika dhidi ya Daesh. Tangu mwaka uliopita serikali
ya Washington imekuwa ikiongoza operesheni za mashambulio ya anga dhidi
ya ngome za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh lakini mashambulio
hayo hayajapata mafanikio yoyote. Siku ya Jumatano iliyopita, msemaji wa
Ikulu ya Marekani Josh Earnest alisema Rais Obama ametoa amri ya
kutumwa askari 450 wa ziada nchini Iraq kwa ajili ya kutoa ushauri kwa
vikosi vya nchi hiyo kutokana na ombi la Waziri Mkuu Haidar al-Abadi.
Askari hao wataifanya idadi ya askari wote wa Marekani walioko nchini
Iraq ifikie 3,550. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon,
hadi sasa nchi hiyo imeshatumia zaidi ya dola bilioni 2.7 katika
operesheni za kijeshi dhidi ya Daesh katika nchi za Iraq na Syria ambazo
ni wastani wa zaidi ya dola milioni tisa kwa siku…/
No comments:
Post a Comment