Saudi Arabia imeendeleza jinai zake za kivita nchini Yemen huku makumi ya raia wasio na hatia wakiuawa katika hujuma za leo.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Yemen, Saba,
katika hujuma ya ndege za kivita za Saudi Arabia leo Ijumaa katika
maeneo mbali mbali ya Yemen hasa mikoa ya Sa'ada, Hajja na Aden, raia
wasiopingua 40 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Ndege za kivita
za Saudi Arabia pia zimedondosha mabomu katika hospitali katika mji wa
Dhamar mbali na kuhujumu pia chuo kikuu mjini humo.
Huku hayo yakijiri makumi ya maelfu ya watu wameandamana
katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a kupinga na kulaani hujuma ya kijeshi ya
Saudi Arabia dhidi ya nchi yao.
Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Taasisi ya Uhuru
ya Yemen, tangu yalipoanza mashambulio ya kivamizi ya Saudia dhidi ya
nchi hiyo Machi 26 mwaka huu ambayo yamefanywa bila ya idhini ya Umoja
wa Mataifa, hadi sasa watu wasiopungua 4,000 wameshauawa na wengine
7,000 kujeruhiwa. Aghalabu ya wahanga wa hujuma hizo zinazoongozwa na
Saudia ni watoto, wanawake na raia wa kawaida wasio na hatia
No comments:
Post a Comment