Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Thursday, 18 June 2015

Ramadhani imeanza leo maeneo mengi ya dunia

Waislamu katika nchi nyingi duniani leo wamenza funga ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Taasisi husika katika nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizo za Kiislamu zilitangaza jana jioni kwamba Alkhamisi ya leo tarehe 18 Juni itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wenye baraka na mtukufu wa Ramadhani ambamo Waislamu hufunga swaumu na kujikurubisha kwa Mola Karima kwa kujipinda kwa ibada na dua.
Hapa nchini Iran Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ilitangaza jana jioni kwamba Leo Alkhamisi ni siku ya kwanza ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo ilisema mwezi mwandamo ulionekana jana jioni na kwamba leo ni tarehe mosi Ramadhani.
Taasisi za kidini katika nchi kama Saudi Arabia, Misri, Sudan, Imarati na Qatar pia zimetangaza siku ya leo kuwa ni tarehe Mosi Ramadhani.
Leo Akhamisi pia imetangazwa kuwa tarehe Mosi Ramadhani katika nchi za Afrika Mashariki.
Idhaa ya Kiswahili ya Redio Tehran inawatakia Waislamu wote mwezi uliojaa baraka wa Ramadhani na tunamuomba Mola Karima atakabali dua na ibada zetu katika mwezi huu.

No comments:

Post a Comment