Askari wa utawala haramu wa Israel wamempiga risasi na
kumuua shahidi Mpalestina katika kijiji kimoja karibu na mji wa Ramallah
katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Abdullah Ghanayem aliyekuwa na umri wa miaka 21 aliuawa shahidi katika Kijiji cha Kufor Malek mapema leo asubuhi.
Duru za Palestina zinadokeza kuwa gari la kijeshi la Israel
limepinduka katika makabaliano hayo na kumuangukia Mpalestina aliyeuawa
shahidi.
Askari wa Israel wamekihujumu kijiji hicho na kuwateka
Wapalestina kadhaa. Jeshi la utawala dhalimu wa Israel huvamia nyumba za
Wapalestina mara kwa mara katika Ukingo wa Magharibi na kuwateka nyara
Wapalestina ambao hupelekwa katika korokoro za kuogofya za utawala huo.
No comments:
Post a Comment