Sunday, 14 June 2015
Iran yatoa radiamali kupinga taarifa ya PGCC
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Iran amepinga taarifa ya hivi karibuni ya Baraza la Ushirikiano la
Ghuba ya Uajemi kuhusu visiwa vitatu vya Iran. Bi Marzieh Afkham amejibu
matamshi hayo ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa kusema
kuwa: Kukaririwa madai yasiyo na msingi hakujakuwa na athari kwa uhakika
wa kihistoria. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema visiwa
vya Bumusa, Tomb Kubwa na Ndogo ni sehemu ya ardhi ya Iran isiyoweza
kutenganishwa. Afkham ameongeza kuwa: Iran inatoa kipaumbele katika
siasa zake kwa suala la kuwa na uhusiano mwema na majirani zake,
uhusiano ambao umejengeka kwa kutoingilia masuala ya nchi nyingine na
kuheshimiana pande mbili na haina kizuizi chochote katika kustawisha na
kupanua mahusiano ya kirafiki. Bi Afkham amesema Iran inakaribisha
kuwepo maelewano na ushirikiano mkubwa wa pande zote na majirani zake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment