Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametahadharisha maafisa wa serikali
yake wanaojihusisha na biashara haramu ya pembe za ndovu akisema
watakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Akizungumza mapema
leo kwenye mkutano wa wawekezaji mjini Nairobi, Rais Kenyatta ameagiza
maafisa wa usalama kuchunguza kesi inayohusiana na kukamatwa kwa shehena
kubwa ya pembe za ndovu huko Thailand mwezi Aprili ambayo inaaminika
kutoka Kenya na kuwafikisha wahusika wote mbele ya vyombo vya sheria.
Pia Rais wa Kenya ameonya wawekezaji na maafisa wa idara za serikali
wanaojihusisha na uingizaji wa bidhaa bandia nchini akisema chuma chao
ki motoni. Kiongozi huyo amesema bidhaa bandia zinazoingizwa Kenya
zinachangia soko la ndani kuporomoka na hivyo kuwafanya vijana wengi
kukosa nafasi za ajira. Pia amesema jmbo hilo linahatarisha usalama wa
taifa kwani bidhaa ghushi zinazoingizwa hazikaguliwi na hivyo kuna
uwezekano wa kuingizwa hata silaha kupitia njia hizo.
Maafisa kadhaa wa idara ya forodha pamoja na wale wa mamlaka ya
ukusanyaji ushuru wamekamatwa na kufikishwa kortini kuhusiana na
biashara haramu ya meno ya tembo
No comments:
Post a Comment