Akiomba mwongozo kwa naibu spika, mbunge wa mtera Mhe.Livingstone
Lusinde ametaka kamati ya uoungozi kuongeza muda wa kujadili tuhuma
zinazojitokeza na hasa zinagusa baadhi ya mawaziri na wabunge wenyewe
ambao wanalalamikiwa.
Katika hatua nyingine kamati ya kudumu ya bunge ya uchumi,viwanda
na biashara ikitoa maoni kuhusu mswada wa marekebisho ya sheria ya ubia
baina ya sekta ya umma na sekta binafsi wa mwaka 2014 imesema changamoto
zinazoikabili serikali ni kutokuwepo kwa sera zinazowalinda wazawa
kushiriki katika uwekezaji nchini.
Wakichangia muswada wa marekebisho ya sheria ya ubia na bina ya
sekta ya umma na sekta binafsi,baadhi ya wabunge wamehoji serikali
inampango gani wa kuwawezesha wawekaji wa ndani kama ambavyo nchi
nyingine zinazoendelea na zisizoendela zinafanya katika kuwajengea uwezo
watu wake.
Awali akiwasilisha muswada huo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu
uwekezaji na uwezeshaji, Mhe.Mary Nagu amesema mapendekeza hayo
yanalenga kuongeza utekelezaji wa miradi ya ubia pamoja na mazingira
yatakayowezesha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kuwekeza
katika miradi ya kiuchumi na kijamii.
No comments:
Post a Comment