GAPCO YAZINDUA KADI MAALUM ZA SAFARI ZITAKAZOWEZESHA DEREVA KUPATA UNAFUU WA BEI YA MAFUTA KATIKA VITUO VYOTE, TANZANIA
Rais
wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akipongezana na
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto) baada
ya kuzindua kadi maalum za Safari za kampuni hiyo zitakazomwezesha
dereva kupata huduma ya mafuta kutoka vituo vyote vya Gapco nchini kwa
unafuu. Wengine (kustoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai,
Ashok Dhar, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara, Ofisa Mtendaji
Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na Mkurugenzi
wa kituo cha Gapco, Barabara ya Nyerere, Muntazir Bharwani.
Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akikabidhi
kadi maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara na
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki baada ya kuzindua kadi
hizo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika
hafla iliyofanyika Kituo cha Mafuta Gapco cha Kamata, Dar es Salaam
jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai,
Ashok Dhar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk.
Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Rais
wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok akionesha kadi maalum
za Safari za Gapco baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika
kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Kadi hizo
zitamwezesha dereva kuweza kupata huduma ya mafuta kwa unafuu kutoka
vityo vyote vya Gapco Tanzania. Kutoka kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu
wa Gapco Tanzania, Vijay Nair, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum
Bisarara, Diwani wa Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto),
Meneja Miradi wa Gapco, Mohit Shirma, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la
makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Meneja
Uendeshaji wa Kadi za Gapco, Shital More akielezea matumizi ya kadi
maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki
(katikati) baada ya kuzindua rasmi kadi hizo zitakazomwezesha dereva
kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika vituo vyote vya Gapco nchini
katika hafla iliyofanyika kituo cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana.
Wengine (kutoka kushoto) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya
Gapco, Dk. Macharia Irungu, Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit
Shirma, Rais wa kampuni ya Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok
Dhar na maofisa wengine wa Gapco.
Diwani
wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa pili kulia) akifurahia
jambo baada ya kuelekezwa matumizi ya kadi maalum za Safari Gapco na
Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit Shirma baada ya kuzindua kadi
hizo, katika kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana.
Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk.
Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa
kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi maalum za Safari
zitakazomuwezesha dereva kupata unafuu wa mafuta kutoka katika vituo
vyote vya Gapco, Dar es Salaam jana.
Diwani wa Kata ya
Kariakoo, Abdulkarim Masamaki akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
hafla ya uzinduzi wa kadi maalum za Safari zitakazomuwezesha dereva
kupata unafuu wa mafuta kutoka katika vituo vyote vya Gapco, Dar es
Salaam jana.
Kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa bidhaa za mafuta nchini,
imezindua programu aminifu kuwezesha wamiliki wa magari kujipatia pointi
wakinunua mafuta ambazo zitawawezesha kupata ‘Mafuta Bure’ Kama faida.
Mpango huu utawanufaisha wakazi wa Dar es Salaam, kwa kuanzia na nchini kote mwakani.
Jerry Slaa, Maya wa Manispaa ya Ilala akizungumza katika sherehe ya
uzinduzi iliyofanyika katika kituo cha GAPCO Kamata jijini Dar es
Salaam alisema: "kuanzishwa kwa programu ya GAPCO Safari kutasaidia
kutatua changamoto za muda mrefu zinazowakabili wamiliki wa magari
nchini. Mfumo huu ni muhimu kuelekea jamii ya kufanya malipo bila fedha
taslimu.”
Slaa alipongeza GAPCO kwa kuwa Kampuni ya kwanza katika sekta ya
mafuta Kurudisha thamani ya fedha kwa wateja wake nakuomba Kampuni
zingine kufuata nyayo za GAPCO.Alibainisha kuwa huduma hii itasaidia
kupunguza kwa ujumla, gharama za mafuta, kupunguza bugudha ya makaratasi
na kusaidia kuendesha biashara kwa ufanisi zaidi.
Slaa aliongeza kwamba maendeleo kama hayo ni muhimu katika
kuboresha uchumi wa nchi kwa kuwa usafiri ni moja ya nguzo muhimu ya
uchumi wa Tanzania. Slaa alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuunga
mkono juhudi hizo ili kuboresha sekta ya usafiri nchini.Dr Macharia
Irungu, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) GAPCO Group alisema GAPCO ina maslahi
mapana katika soko la Afrika Mashariki na inajivunia kuwa na vituo vya
mafuta 63 nchi nzima, na kuifanya GAPCO kuwa moja ya kampuni ya mafuta
inayoongoza.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi kuzindua rasmi mpango, Bw. Ashok Dhar,
Rais wa Reliance Industries Limited India, kampuni mama ya GAPCO
Tanzania Ltd, alisema kuwa mpango huu unawakilisha sehemu ndogo ya faida
ya GAPCO.Bw. Dhar alisema anaimani na Uchumi wa Tanzania, na hivyo
kampuni yake itaendelea kuwekeza zaidi nchini kwa miaka ijayo.
Akifafanua zaidi juu ya programu ya GAPCO Safari, Vijay Nair, Afisa
Uendeshaji (COO) alisema kuwa kadi za Gapco Safari zitakuwa
zinapatikana wakati wowote katika vituo vya mafuta vya GAPCO mkoani Dar
Es Salaam kwa kuanzia.mtendaji alieleza kuwa huduma hiyo ilikuwa wazi
kwa wamiliki binafsi, kampuni na wafanya biashara ya magari.
"Tunataka kuboresha zaidi huduma zetu za uuzaji mafuta kwa wateja
wetu. GAPCO tunaandhisha huduma ya kutoa huduma aminifu ambayo ni
suluhisho kwa wamiliki wa magari nchini kote… Hii ni huduma ya kipekee
tuliyo ianzisha tukiamini kupitia Kauli mbiu ‘……….’," alisema Bw Nair.
No comments:
Post a Comment