MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatarajia kuendesha kampeni
ya siku 60 nchini kuhamasisha jamii kujiunga na huduma za mfuko wa Afya
ya Jamii (CHF/Tika).
Kampeni hiyo ambayo inaanza mwezi huu, itahusisha halmashauri 54, lengo likiwa ni kuingiza watu asilimia 5 kwa kila halmashauri pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya kuboresha huduma hasa upatikanaji wa dawa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (NHIF), Beatus Chijumba, alisema wananchi wakijiunga na mfuko huo wanakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu.
Katika awamu hii ya kwanza ya kampeni halmashauri zitakazofikiwa ni za mikoa ya Kilimanjaro, Ruvuma, Kagera, Kigoma, Iringa, Singida, Tabora, Pwani, Shinyanga, mara, Njombe, Simiyu, Geita, Mtwara, Manyara, Katavi, Mwanza, Rukwa, Arusha, Tanga, Morogoro, Lindi na Mbeya.
“Zoezi hili linafanyika katika mikoa 24 isipokuwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo mfuko utaendesha zoezi maalum kwa vikundi vya wajasiriamali waliopo kwenye vikundi katika halmashauri zote, ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko,” alisema.
Akizungumzia uboreshaji wa huduma huduma hasa upatikanaji wa dawa, Mkurugenzi wa Matibabu na Masuala ya Kiufundi, Dk. Frank Lekey, alisema hilo linawezekana kwa hospitali wanazozihudumia kwa kuwa wanatoa mikopo mbalimbali ikiwemo ya dawa. Mikopo mingine yanayotoa ni ya vifaa tiba, ukarabati wa vituo vya afya na vifaa vya mfumo wa habari (Tehama).

No comments:
Post a Comment