MBUNGE wa Morogoro Vijijini, Dk, Lucy Nkya (CCM), ametaka kujua ni
kwanini wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii hawapewi hisa
inayotokana na miradi iliyowekezwa kupitia michango yao.
Mbunge huyo, alihoji hatua hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la msingi, ambapo alitaka kujua ni kwa nini mifuko hiyo haitoi gawio la faida itokanayo na miradi hiyo kwa wanachama.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, alisema Tanzania ina mifuko sita ya hifadh ya Jamii ambayo huendeshwa kwa misingi ya bima ya jamii ambapo wanachama walio wengi hawachangii wachache waliopatwa na majanga.
“Kutokana na thamani ya mafao yanayotolewa na mifuko kuwa makubwa ukilinganisha na michango, fedha zitokanazo na michango ya wanachama huwekeza katika vitega uchumi kwa lengo kupata fedha zaidi kwa ajili ya kulipa mafao hayo,” alisema.
Alisema hivi sasa mfuko yote ya lazima ya hifadhi ya jamii nchini inafuata mfumo wa ‘Defined Benefit’ ambao misingi yake ni ya bima.
Kabaka alisema katika mfumo huo, mwanachama huahidiwa mafao mbalimbali pamoja na pensheni.
“Kwa mfumo huu mwanachama hapewi hisa kwa sababu ameahidiwa mafao ambayo lazima alipwe bila kujali michango iliwekezwa wapi, kwa sababu hiyo gawio au hasara inayotokana na uwekezaji inachangia moja kwa moja kwenye mfuko husika,” alisema.

No comments:
Post a Comment