Ukawa yabaini Njama za Kuondoa Mjadala
juu Kashfa ya fedha Bilioni 321 za Akaunti Ya Tegeta ESCROW kwa Kutumia
Mgongo Wa Mahakama.
Umoja
wa katiba ya wananchi-Ukawa imebaini kuwepo kwa njama za kutaka kuondoa
mjadala wa wizi wa zaidi ya Bilioni 321 fedha zilizokuwa katika akaunti
ya tegeta ESCROW Bungeni kwa kutumia chombo cha mahakama.
Akizungumza na waandishi wa habari,mwanasheria wa ukawa Mhe.Tundu
Lissu amesema ipo taarifa ya barua kutoka mahakamani inazodai sakata la
ESCROW liko mahakamani hivyo halipaswi kujadiliwa Bungeni,na kusisitiza
hakuna utaratibu wowote mahakama unaoipa mamlaka ya kulieleleza Bunge
jambo la kufanya.
kwa upande wake mwenyekiti mwenza wa ukawa Mhe. James Mbatia
amesema Bunge linahitaji muda wa kutosha kuhakikisha kashfa hiyo
inajadiliwa kwa upana na baada ya uchunguzi wa Ripoti ya PAC kuonyesha
Bunge watakaotuhumiwa swala la kisiasa,kisheria wawajibishwe.
Hivi karibu,naibu spika wa bunge alikabidhi Ripoti ya mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu wizi wa zaidi ya shilingi
Bilioni 321 fedha zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta ESCROW ambao
inadaiwa kuhusisha baadhi ya viongozi mbalimbali wa serikalini.
No comments:
Post a Comment