Monday, 11 May 2020
Sunday, 29 September 2019
Monday, 26 August 2019
Friday, 23 August 2019
Thursday, 22 August 2019
Tuesday, 20 August 2019
Wednesday, 13 December 2017
Sehemu ya ndege ye jeshi la Marekani imeanguka kwenye shule katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan na kuzua upya misukosuko na watu wa eneo hilo.
Sehemu ya ndege ye jeshi la Marekani
imeanguka kwenye shule katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan na kuzua
upya misukosuko na watu wa eneo hilo.
Sehemu hiyo ya dirisha ilianguka kwenye uwanja wa shule na kusabisha majeraha madogo kwa mwanafunnzi mmoja.Kisiwa cha Okinawa kina kambi kuwa zaidi ya jeshi la Marekani nchini Japan.
Jeshi la Marekani lilithibitisha kuwa dorisha kutoka moja ya helikopta zake ilianguka kwenye uwanja wa michezo wa shule iliyo nje ya kambi ya yake ya jeshi la wanahewa.
Tuesday, 24 May 2016
Wazazi ungeni mkono jitihada za Serikali kuimarisha michezo kwa Vijana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezindua mashindano ya Shirikisho
la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE) na
kusisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendeleza na kuimarisha michezo
katika skuli na vyuo nchini.

Aliongeza kuwa kama ilivyofanyika katika kipindi kilichopita na kipindi kijacho jitihada zitaendelea kufanyika kuwahamasisha watoto kupenda michezo na hatimae kuanzisha klabu za michezo mbali mbali maskulini.Katika mnasaba huo, Dk. Shein alitoa wito kwa wazazi kuwahamasisha na kuwashajiisha watoto kupenda michezo na kwa wale ambao wanashiriki michezo kuwaunga mkono kwa kuwa michezo ni muhimu katika makuzi ya mtoto kiafya na hata kumsaidia katika kumjenga katika masomo yake.
Aliwakumbusha wazazi kuwa michezo sio sababu zinazowafanya watoto kuwa watukutu na kwamba tabia hiyo kwa watoto husababishwa na mambo mengine katika jamii hivyo watoto wapewe fursa ya kushiriki michezo kadri inavyowezekana.
Dk. Shein aliitaka jamii kuiangalia michezo katika sura tofauti na huko nyuma ambapo zaidi ilikuwa burudani lakini sasa michezo imekuwa ni sehemu inayotoa ajira nyingi na zenye manufaa kwa vijana hivyo jamii haina budi kushirikiana na Serikali kuimarisha michezo nchini.
Aliongeza kuwa lengo la kuanzisha vuguvugu la michezo maskulini na vyuo lengo lake ni kuibua vipaji na kuviendeleza ili Zanzibar iweze kutoa wanamichezo bora watakaweza kushindana na kushinda hatimae kurejesha hadhi ya Zanzibar katika ramani ya michezo ulimwenguni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kusimamia vyema utekelezaji wa Sera ya Michezo nchini ikiwemo kusimamia vyema maandalizi ya mashindano mbalimbali katika ngazi zote za elimu.
Uzinduzi wa Mashindano hayo ambayo yanajumuisha michezo mbali mbali ikiwemo riadha, netiboli na mpira wa miguu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanamichezo kutoka vyuo mbalimbali Zanzibar.
Thursday, 15 October 2015
Diamond na zari
Mfahamu kwa undani zaidi mwanadada ZARI wa Uganda aliyetibua penzi la WEMA na Diamond. Ni tajiri balaaa! http://www.muungwana.com/2015/10/mfahamu-kwa-undani-zaidi-mwanadada-zari.html
Friday, 25 September 2015
Tuesday, 22 September 2015
MAGUFULI AWAKUNA WANANCHI WA KARAGWE,APIGA PUSH UP JUKWAANI,WANANCHI WASHANGILIA




Waziri amchefua Magufuli
*Aomba Watanzania wamtetee kwa uamuzi atakaochukua
Na Bakari Kimwanga, Muleba
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameahidi kushughulika na mmoja wa mawaziri aliyegawa ranchi za mifugo kiholela.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana, alipohutubia mikutano ya kampeni iliyofanyika katika miji ya Muleba na Kamachumu mkoani Kagera.
Alisema hawezi kukubali kuona wananchi wanaendelea kuteseka wakati watu fulani wanamiliki ranchi hizo, huku migogoro isiyomalizika ikiendelea kufukuta.
Hata hivyo, katuika mkutano huo, Dk. Magufuli hakumtaja waziri huyo wala alikuwa katika serikali ya awamu gani, isipokuwa alisisitiza kupambana naye akiingia madarakani.
“Ninajua hapa kuna mgogoro wa ranchi ya Rutoro ambayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongela amesema anaushughulikia. Nawaambia mkoa wenu una ranchi 52 ambazo zimegawiwa kiajabuajabu.
“Hakuna jambo linalomuumiza kichwa Rais Kikwete, kama uamuzi huu wa mtu mmoja kugawa ovyoovyo maeneo haya kwa watu ambao hawana ng’ombe wala mbuzi…nasema hili hapana.
“Sitawaangusha, tutakwenda kupambana na watu hawa ambao wameharibu,” alisema Dk. Magufuli.
Alisema hayuko tayari kuona wananchi wanaumia kwa makosa yaliyofanywa na watu walioaminiwa katika utendaji serikalini.
“Kama mtanichagua kuwa rais, tutagawa baadhi ya maeneo na kuwapa wananchi ili wapate maeneo ya malisho ya mifugo na kilimo,” alisema Dk. Magufuli.
SOKO LA KAHAWA
Kuhusu soko la kahawa, mgombea huyo alisema anatambua changamoto zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Alisema anashangazwa na bei ya kahawa inayotoka Kagera kwenda Uganda kuwa na soko kubwa, wakati nchini bei imezidi kushuka kila kukicha.
“Ikulu ni ya Magufuli na CCM, wengine wasindikizaji. Msiwasikilize, ninaomba kura zenu zote Watanzania,” alisema.
Alisema anaomba urais kwa ajili ya kuwatumikia wananchi ambao wanaonekana kukatishwa tamaa na baadhi ya watendaji wa serikalini ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao.
AHADI YA MELI
Alisema ahadi iliyotolewa na Rais Kikwete kila ziwa kubwa kuwa na meli iko palepale.
Aliwaasa wananchi wa Kagera kuepuka kauli za wanasiasa kufanya ajenda ya meli kuwa mtaji wa kuombea kura.
TIBAIJUKA APIGA MAGOTI
Katika hatua nyingine, mgombea ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini kupitia CCM, Profesa Anna Tibaijuka, aliwavunja mbavu wananchi baada ya kuomba kura akiwa amepiga magoti.
Akiwa mbele ya Dk. Magufuli, Profesa Tibaijuka aliomba asaidiwe kupata barabara ya lami.
“Ninaomba nikipiga magoti kwako mgombea urais, pamoja na maendeleo mengine kupatikana, naomba barabara ya lami kuelekea Hospitali ya Rubya…yaani imekuwa kero wakati mvua zinapoanza kunyesha,” alisema Profesa Tibaijuka huku akishangiliwa.
AOMBA KUTETEWA
Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli, amewaomba Watanzania wamtetee kutokana na uamuzi atakaochukua dhidi ya viwanda vya umma visivyoendelezwa.
Alisema kutokana na uamuzi huo, watu wasiomtakia mema wageuza ajenda hiyo na kudai atawanyanyasa wafanyabiashara.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano aliofanya Jimbo la Bukoba Vijijini jana na kusema dhamira ya kuchukua viwanda visivyoendelezwa ipo palepale na hatorudi nyuma.
“Watanzia niteteeni kwa kunichagua kwa kura nyingi, niliposema tutachukua viwanda vilivyoshindwa kuendelezwa, kuna watu wanageuza maneno na kusema nitawaonea wauza maduka.
“Siwezi kufanya hivyo, wenye maduka wengi wao ni wanyonge ambao mimi ndiyo mtetezi wao wa kweli.
“Leo viwanda vyote walivyobinafsishiwa watu, wameshindwa kuviendeleza, vimegeuka maghala ya mbuzi… hapa Bukoba tulikuwa na kiwanda cha chai kimekufa, vijana wetu hawana ajira wanaishi maisha magumu.
“Najua ninasimama hapa nikizungumza mafisadi hawanipendi na ninawaomba wana Bukoba na Watanzania mniombee.
“Najua hata hapa Bukoba wapo, wamekuwa wakileta hela zao ili msinichague, hela zao kuleni na mnichague kwa wingi,” alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa.
MAUAJI
Dk. Magufuli alilaani mauaji ya watu kwa kukatwa makoromeo, huku akisema suala hilo ni lazima likome kwani haliendani na ubinadamu.
“Kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake, anatakiwa kulaani mauji ya aina hii. Leo mtu unatoka kupata lubisi unakutana na mtu anakukata koromeo, huu ni utamaduni gani ndugu zangu?” alihoji Dk. Magufuli.
Mtanzania
Monday, 21 September 2015
Saturday, 19 September 2015
Tujivunie Zanzibar
Tunajivunia kufanya kazi na rasilimali bora za nchi yetu, Ni watu, Ni Wazanzibari! Tujivunie Zanzibar.
________________________________________
Zanzibar is a unique part of the world! This is said by UNESCO, by tourists, and we all know it! This is the place where we live and work in peace, security and faith! Every year hundreds of thousands of tourists from around the globe enjoy being in our country! We are blessed to live here every day, every single day should bring more hope for us and our families so we could enjoy Zanzibar throughout the time!
We are proud to work for the best assets our country has: It's people, It's Zanzibaris ! Let’s be proud of Zanzibar!
Mgombea ubunge wa CUF ahamia CCM
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimepasuka wilayani Mafia, mkoani Pwani,
baada ya aliyeidhinishwa kugombea ubunge Mafia, Mohammed Albadawi,
kuhama chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Albadawi pamoja na kuidhinishwa na CUF kuwa mgombea wake katika jimbo hilo, siku chache baadaye alikatwa na nafasi yake hiyo kupewa aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM lakini alishindwa kwenye kura za maoni, Omary Kimbau.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, kada huyo wa zamani wa CUF alisema chama hicho kimemdhalilisha na kumshusha thamani kwa kumuondoa na kumuweka mwingine aliyeshindwa alikotoka.
“Mimi nilikuwa kada wa CUF, hii ni mara ya kwanza kuhutubia mkutano wa CCM, nimefanya kazi kubwa ya kukinadi CUF lakini kwa sasa sina hamu kabisa na chama hicho,” alisema.
Alisema alikuwa ni mmoja wa wanachama wa CUF waliochukua fomu za kuwania ubunge ambapo Kimbau aliyepewa nafasi hiyo ya kugombea ubunge, kwa upande wake alichukua fomu kuwania nafasi hiyo kupitia CCM.
Alisema katika mchakato wa ndani wa chama chake, alipitishwa na Baraza Kuu la CUF ikiwa ni pamoja na kupigiwa simu na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, akimtaarifu kuwa amepita.
Alisema wakati mchakato wa kura za maoni ukiendelea CUF, kwa upande wa CCM, Kimbau alipigwa chini baada ya kupata nafasi ya pili na kukimbilia CUF ambako walimpatia nafasi hiyo ya kuwania ubunge Mafia na kumkata Albadawi.
“Nilishinda kabisa kura za maoni nilipata kura 99 mwenzangu alipata kura nne, lakini kutokana na mchezo wa biashara, Kimbau akafanya anavyofanya mimi nikatolewa,” alisisitiza.
“Nawaambia leo walichokifanya ni upumbavu, na nachukua fursa hii kuwaambia ndugu zangu hapa hakuna CUF tena, kura zote za ubunge, urais na udiwani ipeni CCM kwa sababu kiongozi yeyote aliyepata nafasi kwa dhuluma hawezi kuwatumikia wananchi
Albadawi pamoja na kuidhinishwa na CUF kuwa mgombea wake katika jimbo hilo, siku chache baadaye alikatwa na nafasi yake hiyo kupewa aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM lakini alishindwa kwenye kura za maoni, Omary Kimbau.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, kada huyo wa zamani wa CUF alisema chama hicho kimemdhalilisha na kumshusha thamani kwa kumuondoa na kumuweka mwingine aliyeshindwa alikotoka.
“Mimi nilikuwa kada wa CUF, hii ni mara ya kwanza kuhutubia mkutano wa CCM, nimefanya kazi kubwa ya kukinadi CUF lakini kwa sasa sina hamu kabisa na chama hicho,” alisema.
Alisema alikuwa ni mmoja wa wanachama wa CUF waliochukua fomu za kuwania ubunge ambapo Kimbau aliyepewa nafasi hiyo ya kugombea ubunge, kwa upande wake alichukua fomu kuwania nafasi hiyo kupitia CCM.
Alisema katika mchakato wa ndani wa chama chake, alipitishwa na Baraza Kuu la CUF ikiwa ni pamoja na kupigiwa simu na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, akimtaarifu kuwa amepita.
Alisema wakati mchakato wa kura za maoni ukiendelea CUF, kwa upande wa CCM, Kimbau alipigwa chini baada ya kupata nafasi ya pili na kukimbilia CUF ambako walimpatia nafasi hiyo ya kuwania ubunge Mafia na kumkata Albadawi.
“Nilishinda kabisa kura za maoni nilipata kura 99 mwenzangu alipata kura nne, lakini kutokana na mchezo wa biashara, Kimbau akafanya anavyofanya mimi nikatolewa,” alisisitiza.
“Nawaambia leo walichokifanya ni upumbavu, na nachukua fursa hii kuwaambia ndugu zangu hapa hakuna CUF tena, kura zote za ubunge, urais na udiwani ipeni CCM kwa sababu kiongozi yeyote aliyepata nafasi kwa dhuluma hawezi kuwatumikia wananchi
AJALI YA LORI YAUA DEREVA SEKENKE, SINGIDA
Mmoja wa mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.
Thursday, 16 July 2015
HON: SALEH ALI ABDALLAH AKIWA WILAYA YA MJINI KATIKA ZOEZI LAUCHUKUAJI FORM YA KUGOMBANIA UWAKILISHI JIMBO LA KIKWAJUNI
AKIWA NA WAANDISHI WA HABARI LEO ALITOA AZMA YAKE YA KUCHUKUA FORM NI KUONDOA CHANGAMOTO ZA VIJANA BAADA YA MUMUONA MUHESHIMIWA MUWAKILISHI WA JIMBO LA KIKWAJUNI KUSHINDWA NA CHANGAMOTO HIZO
Subscribe to:
Posts (Atom)