CHAMA cha Wananchi (CUF) kimepasuka wilayani Mafia, mkoani Pwani,
baada ya aliyeidhinishwa kugombea ubunge Mafia, Mohammed Albadawi,
kuhama chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Albadawi pamoja na kuidhinishwa na CUF kuwa mgombea wake katika jimbo
hilo, siku chache baadaye alikatwa na nafasi yake hiyo kupewa aliyekuwa
mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM lakini alishindwa kwenye kura
za maoni, Omary Kimbau.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais
kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, kada huyo wa zamani wa CUF alisema
chama hicho kimemdhalilisha na kumshusha thamani kwa kumuondoa na
kumuweka mwingine aliyeshindwa alikotoka.
“Mimi nilikuwa kada wa CUF, hii ni mara ya kwanza kuhutubia mkutano
wa CCM, nimefanya kazi kubwa ya kukinadi CUF lakini kwa sasa sina hamu
kabisa na chama hicho,” alisema.
Alisema alikuwa ni mmoja wa wanachama wa CUF waliochukua fomu za
kuwania ubunge ambapo Kimbau aliyepewa nafasi hiyo ya kugombea ubunge,
kwa upande wake alichukua fomu kuwania nafasi hiyo kupitia CCM.
Alisema katika mchakato wa ndani wa chama chake, alipitishwa na
Baraza Kuu la CUF ikiwa ni pamoja na kupigiwa simu na Katibu Mkuu wa
chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, akimtaarifu kuwa amepita.
Alisema wakati mchakato wa kura za maoni ukiendelea CUF, kwa upande
wa CCM, Kimbau alipigwa chini baada ya kupata nafasi ya pili na
kukimbilia CUF ambako walimpatia nafasi hiyo ya kuwania ubunge Mafia na
kumkata Albadawi.
“Nilishinda kabisa kura za maoni nilipata kura 99 mwenzangu alipata
kura nne, lakini kutokana na mchezo wa biashara, Kimbau akafanya
anavyofanya mimi nikatolewa,” alisisitiza.
“Nawaambia leo walichokifanya ni upumbavu, na nachukua fursa hii
kuwaambia ndugu zangu hapa hakuna CUF tena, kura zote za ubunge, urais
na udiwani ipeni CCM kwa sababu kiongozi yeyote aliyepata nafasi kwa
dhuluma hawezi kuwatumikia wananchi
No comments:
Post a Comment