Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Wednesday, 14 January 2015

Boko Haram yawafanya maelfu wakimbilie Chad

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mshambulizi ya hivi karibuni ya kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria yamesababisha watu zaidi ya elfu 11 kukimbilia Chad katika siku kadhaa zilizopita. Kundi la Boko Haram tarehe 3 mwezi huu liliushambulia mji wa Baga unaopatikana katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria na kisha kuuteketeza mji huo na vitongoji vyake visivyopungua 16. Watu wapatao elfu ishirini wanaaminika kuzihama nyumba zao katika mji wa Baga tangu kundi la Boko Haram liushambulie mji huo mapema mwezi huu. Ofisi ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) jana ilitangaza kuwa raia wapatao 11,320 wamewasili katika nchi jirani ya Chad. William Spindler, msemaji wa UNHCR amesema kuwa, asilimia 60 ya raia wapya waliowasili nchini Chad walikuwa ni wanawake na watoto na kwamba watoto 84 wasio na mtu yoyote aliyefuatana nao pia wamewasili nchini Chad. Ravina Shamdasani msemaji wa ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR) ameeleza kuwa ni wazi kwamba mauaji ya umati ya raia na kuwalazimisha watu kuhama kwa nguvu vimetokea katika mji wa Baga nchini Nigeria.

No comments:

Post a Comment