Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Sunday, 26 October 2014

SOBER HOUSE RECOVERY COMMUNITY ZANZIBAR IKIENDELEA NA JUHUDI ZA KUTOA TAALUMA ZA KUJIKINGA NA UTUMIZI WA MADAWA YA KULEVYA KATIKA SULE ZA SECONDARI MJINI ZANZIBAR HII NI BEN-BELLA GIRLS SCHOOL

IKIWA NI MOJA YA MUENDELEZO WA UTOJI ELIMU KUHUSU ATHARI ZA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA , KATIBU MKUU WA UMOJA WA SOBER HOUSE RECOVERY COMMUNITY ZANZIBAR ABDULRAHMAN ABDULLAH AKITOA ELIMU  NA KUELEZA ATHARI ZA MADAWA YA KULEVYA KATIKA SKULI YA SECONARI BEN BELLA

ZOEZI HILO LIKIWA LINAENDELEA KAKIKA MASHULE YOTE  YA SECONDARI KATIBU MKUU  (ABDUL-RAHMAN ABDULLAH ) ANATOA WITO KWA WAZAZI ,WALIMU NA WALEZI KUCHUKUA JUHUDI ZA KUWAFATILIA WATOTO KWANI IMEONEKANA IDADI YA  UTUMIAJI WA MADAWA YAKULEVYA INAZIDI SIKU HADI  SIKU NCHINI TANZANIA MPAKA KUFIKIA ASILIMIA 25% YA IDADI YA WANANCHI NA KUPUNGUZA NGUVUKAZI AMBAZO NIMUHIMU KATIKA JAMII                    

Tunisia holds first election under new constitution

Tunisia is voting to elect its first full parliament under a new constitution passed earlier this year.
The election is one of the final stages in the political transition which followed the ousting of authoritarian leader Zine al-Abidine Ben Ali in 2011.
There are no opinion polls, but the moderate Islamist Ennahda party, which won Tunisia's last national election in 2011, is expected to do well.
Its main rival is likely to be the liberal Nidaa Tounes (Tunisia's Call).
Most of the major parties have vowed to tackle Tunisia's high unemployment and to reinvigorate its economy.
Tunisia is seen as the birthplace of the "Arab Spring" - the pro-democracy movement which sought to replace autocratic governments in several Arab countries.
Tunisia is considered to have had the most successful outcome, with relatively low levels of violence.
However, radical groups within Tunisia have threatened to disrupt the elections and on Thursday militants shot a policeman on the outskirts of the capital, Tunis.

Ebola outbreak: US nurse criticises quarantine treatment

A nurse quarantined on her return to the US from treating Ebola patients in Sierra Leone has criticised the way she was dealt with at Newark airport.

Kaci Hickox said the experience was frightening and could deter other health workers from travelling to West Africa to help tackle the Ebola virus.

Illinois has become the third state after New York and New Jersey to impose stricter quarantine rules.

Meanwhile the US ambassador to the United Nations is to visit West Africa.

Samantha Power will travel to Guinea on Sunday, continuing later to Liberia and Sierra Leone - the three worst-hit countries.

"For me the benefits of having first hand knowledge of what is happening in these countries gravely outweighs the almost nonexistent risk of actually travelling to these countries, provided I take the proper precautions," she said on Saturday.

She said she hoped her trip would "draw attention to the need for increased support for the international response".

The White House has expressed concern that strict quarantine restrictions such as those imposed in New York, New Jersey and Illinois could put off aid workers and others travelling to West Africa to help mitigate the crisis at its source.

More than 10,000 people have contracted the Ebola virus, with 4,922 deaths, according to the World Health Organization's latest figures.

Only 27 of the cases have occurred outside Sierra Leone, Liberia and Guinea.

Thursday, 23 October 2014

HADITHI FUPI YENYE MAFUNZO KWA WANA NDOA


Siku moja niliingia nyumbani nikamkuta mke wangu akiniandalia chakula cha usiku. Nilimshika mkono na kumwambia: “Nina jambo ninalotaka kukueleza.” Alikaa na kunisikiliza kwa makini. Dalili za wasiwasi nilikuwa nikizishuhudia machoni mwake. Ghafla nilijikuta katika hali ya kushindwa kukifungua kinywa changu.
Lakini ilikuwa ni lazima ajue ninachokifikiria, hivyo nilipiga moyo konde, nikamwambia kwa upole: “Ninataka tuachane.” Hakuonekana kuudhika kwa hoja niliyokuwa nimeiwasilisha mbele yake, bali aliniuliza kwa sauti ya upole kabisa: “Kwa nini?” Nilijaribu kulikwepa hilo swali, hivyo
alighadhibika sana na kuniambia kwa sauti ya juu: “Wewe si mwanaume!” Usiku ule hatukusemeshana, na muda wote alikuwa akilia. Nilitambua kuwa alitaka kujua kitu gani kimetokea katika ndoa yetu. Lakini sikuweza kumpa jibu lenye kuridhisha; kwa sababu sikuwa na mapenzi naye tena, moyo wangu ulikuwa umetekwa na binti mwingine aitwaye Jane. Nilimsikitikia sana!
Huku nikiwa na hisia za hatia moyoni mwangu, niliandika pendekezo la
talaka ambalo lilieleza kuwa atachukua nyumba yetu, gari na shea ya asilimia 30 ya kampuni yangu. Mke wangu aliitazama karatasi hiyo kisha akaichana na kuitupa kwenye ndoo ya takataka.
Huyu ni mwanamke aliyekuwa ameishi nami kwa muda wa miaka kumi alikuwa
amegeuka kuwa kama mgeni kwangu. Nilisikitika sana na kumuomba radhi kwa kumpotezea muda, rasilimali na nguvu zake lakini sikuweza kutengua kauli yangu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Jane na nilikuwa nimezama kweli kweli ndani ya huba lake na kuwa teja wa penzi lake. Hatimaye alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo nilikuwa nikitarajia kuliona.
Kilio chake kwangu kilikuwa kama faraja. Wazo la talaka lililonitawala kwa wiki kadhaa lilikuwa likizidi kupata nguvu na sasa lilionekana kuwa wazi kabisa. Siku iliyofuata nilirudi nyumbani nikiwa nimechelewa na kumkuta akiandika kiandika kitu mezani. Sikutaka kula chochote zaidi ya kuelekea moja kwa moja kitandani kwa sababu nilikuwa nimechoka sana kutokana na mishemishe za siku hiyo nikiwa na Jane. Niliposhtuka, bado alikuwa hajatoka mezani. Sikujali hata kidogo, nikageuka na kuendelea kuuchapa usingizi. Asubuhi alinipatia masharti ya talaka: hakutaka
mali yoyote kutoka kwangu, bali alitaka kuwe na muhula wa mwezi mmoja kabla ya talaka.
Alitaka kwamba katika kipindi hicho tujaribukuishi kama kawaida kwa kadiri iwezekanavyo. Hoja yake ilikuwa wazi: mtoto wetu alitarajia kufanya mitihani ya shule ndani ya mwezi huo na hakutaka tumchanganye kwa tukio la talaka. Hili nililikubali. Lakini alikuwa na nyongeza:
alinitaka nikumbuke siku ya ndoa yetu nilipomnyanyua kumpeleka chumbani kwetu. Alitaka kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mzima niwe nambeba kila siku asubuhi kumtoa chumbani mpaka mbele ya mlango wa nje ya nyumba. Nilihisi kuwa alikuwa ameshikwa na wendawazimu. Nilikubali ombi lake kwa sababu niliona kuwa mwezi mmoja sio kitu, kwani nilitaka tuachane.
Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya talaka yaliyotolewa na mke wangu. Alicheka sana na kuona kuwa ni upuuzi. “Hata akitumia hila gani lazima apewe talaka,” alisema Jane kwa masihara. Tangu nilipoelezea nia yangu ya kutaka kuachana naye, hatukuwa na uhusiano wa kimwili na mke wangu. Hivyo nilipombeba siku ya kwanza, sote tulionekana kutokuwa na uchangamfu. Mtoto wetu alifurahi na kupiga makofi: “Baba amembeba mama”. Kauli yake ilinipa maumivu moyoni. Kutoka chumbani mpaka barazani, kisha mlangoni, nilitembea mita kumi nikiwa nimembeba mikononi mwangu. Aliyafumba macho yake na kuniambia
kwa upole na ulaini: “Usimwambie mtoto wetu kama tunaachana.” Nilikubali kwa kutikisha kichwa huku
nikiwa nimefadhaika. Nilipofika nje
nilimshusha akaenda kituoni kusubiri basi, nami nikachukua gari langu na kwenda ofisini nikiwa peke yangu. Siku ya pili tulijaribu kutoonesha hali yoyote ya mifarakano. Aliegemea kifuani kwangu nikahisi manukato mazuri ya blauzi yake. Nilibaini kuwa sikuwa nimemtazama vizuri mke wangu kwa muda mrefu. Uso wake ulikuwa umeanza kuwa na mikunjo na nywele zake zilikuwa zimeanza kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa imemfanya achoke. Kwa dakika kadhaa niliduwaa na kuwaza kile nilichokuwa nimemfanyia.
Siku ya nne nilipombeba nilihisi aina ya
ukaribu na mvuto ikirejea. Huyu ni mwanamke aliyekuwa amenipa miaka
kumi ya uhai na maisha yake. Siku ya tano na ya sita, kwa mara nyingine, niliona hali ya ukaribu na mvuto fulani ikirejea kati yetu. Sikumsimulia Jane kuhusu hali hii. Kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo nilivyozidi wepesi wa kumbeba. Yumkini ilisababishwa na
ile hali ya kumbeba kila siku kiasi cha kumuona kuwa ni mwepesi. Asubuhi moja alikuwa akichagua nguo ya kuvaa. Alijaribu nguo kadhaa lakini hakupata
inayomfaa. Alishusha pumzi na kusema: “Nguo zangu zote hazinienei,
zimekuwa kubwa”. Nilibaini kuwa alikuwa
amekonda na ndiyo maana niliweza kumbeba kwa urahisi. Nilisikitika kwa
sababu nilihisi kuwa alikuwa amebeba mambo mengi moyoni mwake. Hivyo nilimsogelea na kukipapasa kichwa chake. Ni wakati huo ambapo mtoto wetu aliingia na kusema: “Baba sasa ni muda wa kumbeba mama”. Tukio la kumuona
baba yake akiwa amembeba mama yake
lilimuathiri na kuwa sehemu muhimu sana ya maisha yake. Mke wangu alimuita na kumkumbatia kwa upendo.
Niligeuza uso wangu pembeni, sikutaka
kuangalia tukio hilo nisije nikabadilisha uamuzi wangu wa talaka. Nilimnyanyua na kumbeba mke wangu,nikatembea kutoka chumbani, sebuleni mpaka nje. Aliizungusha mikono yake mizuri shingoni kwangu, nami nikamshikilia vizuri; ilikuwa kana kwamba ni siku ile ya harusi yetu. Lakini wepesi wa mwili wake ulinifanya niwe mwenye huzuni. Siku ya
mwisho nilipombeba niliingiwa na uzito
wa kupiga hatua. Wakati huo mtoto wetu tayari alikuwa shule. Nilimshikilia vizuri na kusema: “Sikuwa nimejua kuwa maisha yetu yamekosa mvuto”. Niliwasha gari kuelekea ofisini, niliamua kupita kwa Jane.
Nilipofika nilitoka haraka bila hata kuubana mlango wa gari. Nilikuwa na wasiwasi nisije nikaghairi nia yangu…
Nikapandisha ngazi. Jane alipofungua
mlango nilimwambia: “Samahani Jane, sitaki kuachana na mke wangu”. Alinitazama kwa mshtuko na kunigusa kwenye paji la uso. “Una homa?” alisema. Niliutoa mkono wake na kumwambia: “Samahani Jane, sitaki kumuacha mke wangu. Yawezekana maisha yangu na mke wangu yalikosa uchangamfu kwa sababu hatukuwa karibu, sio kwa sababu hatukupendana. Sasa nimebaini kwamba kwa kuwa nilimbeba siku ya ndoa yetu, ninapaswa kuendelea kufanya hivyo mpaka kifo kitutengenishe.” Jane alionekana kushtuka sana. Alinizaba kibao, akaubamiza mlango na kuanza kulia. Nilimuacha nikapanda gari na kuondoka. Njiani nilipita kwenye duka la maua nikaagiza shada la maua kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza ujumbe unaotakiwa kuandikwa juu ya kadi nikatabasamu na kumwambia aandike: “Kila siku asubuhi nitakubeba mpaka kifo kitakapotutenga nisha”.
Jioni nilifika nyumbani nikiwa na maua mkononi, tabasamu usoni, nikapandisha ngazi mpaka ndani. Nilipofika chumbani mke wangu alikuwa amelala akiwa amefariki dunia. Kumbe alikuwa akipambana na KANSA kwa miezi kadhaa lakini sikujua kwa sababu nilikuwa nimetekwa na Jane. Bila mimi kufahamu, kumbe marehemu mke wangu alijua kwamba muda si mrefu atafariki dunia na alitaka kuniokoa dhidi ya fikra yoyote mbaya kutoka kwa mtoto wetu kama tungeachana muda mfupi kabla ya kifo chake. Angalau machoni mwa mwanangu naonekana kuwa mume
mwenye upendo…
WAPENDANAO NATAKA MJIFUNZE
(1) Wengi wanatengana si kwa sababu hawapendani, bali hawapeani muda wa kusikilizana.
(2)Wengi wanaamini ukiachana na mpendwa wako ni lazima muwe maadui.
(3)Busara ndani ya pendo ni zaidi ya mali na pesa.....
(4) Kaa karibu na mkeo na familia yako muda wote ili ujue nini kinawasibu na uwasaidie katika utatuzi.
(5)Mkeo/mmeo hupenda wewe uwe na furaha hata kama yeye anaumia.

Sunday, 19 October 2014

Gereza yavamiwa Kivu Kaskazini

Watu waliokuwa na silaha wamevamia gereza mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo na kuwaachilia huru wafungwa kama 400.


Uvamizi huo ulitokea Jumamosi usiku katika mji wa Butembo katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Msemaji wa serikali ya Congo, Lambert Mende, alithibitisha kuwa gereza ilivamiwa lakini aliiambia BBC kwamba bado wanachunguza vipi shambulio hilo lilifanywa.

Kumetokea mashambulio katika jimbo la Kivu Kaskazini katika siku 10 zilizopita - mashambulio yanayodaiwa kufanywa na wapiganaji wa ADF kutoka Uganda.

Huku nyuma, afisa wa haki za kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa amelaani hatua ya Jamhuri ya Demokrasi ya congo kumfukuza nchini mwakilishi wao. Scott Campbell alitangazwa Alkhamisi kuwa hatakiwi kuwepo nchini DRC.

Katika taarifa yake mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na haki za kibinaadamu, Zeid Raad al-Hussein, alisema wafanyakazi wengine wawili wa Umoja wa Mataifa piya wametishwa vikali.

Kufukuzwa kwa Scott Campbell kulitangazwa siku moja baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kutuhumu kuwa polisi wa Congo wanafanya vitendo vinavyokiuka sana haki za kibinaadamu

JE UNA SIMU YA ANDROID IKIWA JIBU NDIO KING'ARO ENTERPRISES WANAKULETEA APPLIATION YA KUDOWNLOAD APP,GAME,MOVIES ZA KULIPIA KATIKA PLAY STORE NA MARKET FOR FREE


JE UNA SIMU YA ANDROID IKIWA JIBU NDIO KING'ARO ENTERPRISES WANAKULETEA APPLIATION YA KUDOWNLOAD APP,GAME,MOVIES ZA KULIPIA KATIKA PLAY STORE NA MARKET FOR FREE

jinsi ya kupata na kudownload application ambazo zinalipiwa kwenye Google play bure na zenye latest version.

HATUA YA KWANZA:
-download application inaitwa APTOID inapatikana katika link hii

http://m.aptoide.com/installer?lang=EN

au fanya hivi:-nenda kwenye brower yoyote ukaandike APTOIDE then bonyeza search....STORE,au unaweza kuclick ile ya utaona sehemu pameandikwa install aptoide na idounload then istall

HATUA YA PILI
-Kuchua karatasi na pen then nenda kwenye PLAY STORE ...andika majina ya application za kulipia ambazo unazitaka.....ukimaliza nenda kafungue .... application yako ya APTOIDE ulioidownload.....ikifunguka ipo kama play store.....kwa juu upande wa kulia kunasehemu pa kusearch....eeehee kabla ya hivyo vidoti vitatu....paclick..... then unakumbuka majina ulioandika chini ya application ambazo unazitaka haya andika hapo then search itakuja hapo na utaidownload ......isipoonekana nenda kwa chini kidogo utakuta pameandikwa SEARCH OTHER STORES nenda pa click itakuletea complete action using.........
changua brower yoyote hapo.....zitakuja hapo angalia aina ya application unayoitafuta.....angalia yenye wingi wa kudownloduiwa....then click install .....HIVYO NDO JINSI YA KUDOWNLOAD application za kulipia BURE.

JAMBO LA MWISHO JINSI YA KUFANYA SCANNING ya document kwa kutumia simu yako ya android HAINA HAJA ya kutoa ELFU MOJA ya kufanya scanning kwenye INTERNET CAFE ....haya fanya hivi.....nenda kwenye application ya APTOIDE kama nilivyokufundisha hapo juu nenda katafute application inaitwa CAMSCANNER PREMIUM kwenye google play ni dola 5 ila nimekufundisha jinsi ya kuipata bure ......ukishaidownload ifungue then utaona humo humo kuna sehemu ya camera .... haya sasa chukua cheti chako au document yoyote....ipinge picha kutumia hiyo application ....ukimaliza itakuletea uiweke vizuri then kwa chini kulia kunasehemu ipo kama tiki.....haya pa click hapo itakuscania document then itasave kwenye simu tayali kuituma kwenye emails kwa maelezo zaid unaweza kuchangia tzs 1000 vocha katika no +255776645900 au +255652331374 utapata maelekezo sahihi na kukuza technology zanzibar by king'aro enterprises zanzibar ......thank video is coming soon

VIFAA VYA EBOLA KUINGIA MJINI ZANZIBAR

 
Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha THERMAL SCANNER kwa ajili ya kuchunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.

Kifaa hicho kilichowekwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kitatumika kwa ajili ya kuwachunguza zaidi Wageni ambao watatoka katika nchi zilizoathiriwa na Ugonjwa wa Ebola.

Akikabidhi kifaa hicho Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni amesema THEMO SKAN kitasaidia katika kuwabaini watu ambao wameathirika au kuwa na dalili za Ungojwa wa Ebola na kuchukuliwa hatua zaidi.

Dkt Salma amesema iwapo mgonjwa atabainika hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Chumbuni ambacho kimetayarishwa kwa ajili hiyo.


Aidha Dkt Salma amefahamisha kuwa Kituo cha Afya cha Chumbuni kimetengwa kama eneo litakalotumika kwa ajili ya Matibabu kwa mgonjwa atakayebainika kuambukizwa Ugonjwa wa Ebola nchini.

Amesema Wizara ya Afya katika kukabiliana na Ugonjwa huo wa kuambukiza imekuwa ikifanya Jitihada mbalimbali za kutoa elimu na njia mbali mbali za kinga kabla ya Zanzibar kuathirika na Ebola.

Amesema licha ya Vifaa hivyo vilivyotolewa Vifaa vingine vitakuja wiki inayokuja ili viendelee kutumika katika maeneo ya Bandarini na Viwanja vya ndege Unguja na Pemba

Dkt. Salma amesema Ugonjwa huo haujaingia nchini bali Serikali inajiandaa na juhudi zake za kukabiliana na Ugonjwa huo ili usiweze kuingia na kuathiri Zanzibar