Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Wednesday, 13 December 2017

Sehemu ya ndege ye jeshi la Marekani imeanguka kwenye shule katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan na kuzua upya misukosuko na watu wa eneo hilo.


 Sehemu ya ndege ye jeshi la Marekani imeanguka kwenye shule katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan na kuzua upya misukosuko na watu wa eneo hilo.
Sehemu hiyo ya dirisha ilianguka kwenye uwanja wa shule na kusabisha majeraha madogo kwa mwanafunnzi mmoja.
  • Mtu aliyeundia ndege juu ya paa la nyumba yake India
Kisiwa cha Okinawa kina kambi kuwa zaidi ya jeshi la Marekani nchini Japan.
Haki miliki ya picha Hulton Archive
Image caption Sehemu ya helikopta ya jeshi la Marekani yaanguka shuleni Japan
Katika miaka ya hivi karibuni, ajali kadha na visa vya uhalifu vimesababisha kuwepo upinzani dhidi ya kambi hiyo ya Marekani.
Jeshi la Marekani lilithibitisha kuwa dorisha kutoka moja ya helikopta zake ilianguka kwenye uwanja wa michezo wa shule iliyo nje ya kambi ya yake ya jeshi la wanahewa.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gavana wa Okinawa Takeshi Onaga aonyesha picha ya dirisha iliyoanguka shuleni

Tuesday, 24 May 2016

Wazazi ungeni mkono jitihada za Serikali kuimarisha michezo kwa Vijana

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezindua mashindano ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE) na kusisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendeleza na kuimarisha michezo katika skuli na vyuo nchini.
Wazazi ungeni mkono jitihada za Serikali kuimarisha michezo kwa Vijana.
Katika kutekeleza azma hiyo alibainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali imepanga kufundisha somo la michezo katika skuli 6 za sekondari ambapo kati hizo Unguja zimechaguliwa skuli 4 wakati Pemba skuli 2Sambamba na mpango huo, Dk. Shein alifafanua kuwa tangu uongozi wa Awamu ya Saba ulipoingia madarakani tayari imeshawapatia mafunzo ya michezo walimu 574 ambao wanatumika kufundisha somo la michezo maskulini.
Aliongeza kuwa kama ilivyofanyika katika kipindi kilichopita na kipindi kijacho jitihada zitaendelea kufanyika kuwahamasisha watoto kupenda michezo na hatimae kuanzisha klabu za michezo mbali mbali maskulini.Katika mnasaba huo, Dk. Shein alitoa wito kwa wazazi kuwahamasisha na kuwashajiisha watoto kupenda michezo na kwa wale ambao wanashiriki michezo kuwaunga mkono kwa kuwa michezo ni muhimu katika makuzi ya mtoto kiafya na hata kumsaidia katika kumjenga katika masomo yake.
Aliwakumbusha wazazi kuwa michezo sio sababu zinazowafanya watoto kuwa watukutu na kwamba tabia hiyo kwa watoto husababishwa na mambo mengine katika jamii hivyo watoto wapewe fursa ya kushiriki michezo kadri inavyowezekana.
Dk. Shein aliitaka jamii kuiangalia michezo katika sura tofauti na huko nyuma ambapo zaidi ilikuwa burudani lakini sasa michezo imekuwa ni sehemu inayotoa ajira nyingi na zenye manufaa kwa vijana hivyo jamii haina budi kushirikiana na Serikali kuimarisha michezo nchini.
Aliongeza kuwa lengo la kuanzisha vuguvugu la michezo maskulini na vyuo lengo lake ni kuibua vipaji na kuviendeleza ili Zanzibar iweze kutoa wanamichezo bora watakaweza kushindana na kushinda hatimae kurejesha hadhi ya Zanzibar katika ramani ya michezo ulimwenguni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kusimamia vyema utekelezaji wa Sera ya Michezo nchini ikiwemo kusimamia vyema maandalizi ya mashindano mbalimbali katika ngazi zote za elimu.
Uzinduzi wa Mashindano hayo ambayo yanajumuisha michezo mbali mbali ikiwemo riadha, netiboli na mpira wa miguu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanamichezo kutoka vyuo mbalimbali Zanzibar.

Thursday, 15 October 2015

Diamond na zari

Mfahamu kwa undani zaidi mwanadada ZARI wa Uganda aliyetibua penzi la WEMA na Diamond. Ni tajiri balaaa! http://www.muungwana.com/2015/10/mfahamu-kwa-undani-zaidi-mwanadada-zari.html

Tuesday, 22 September 2015

MAGUFULI AWAKUNA WANANCHI WA KARAGWE,APIGA PUSH UP JUKWAANI,WANANCHI WASHANGILIA

 Kuonyesha kwamba yuko fiti ana anastahili kupewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya kipindi cha tano,Dkt John Pombe Magufuli aliwashangaza wananchi wa mji huo kwa kupiga push up zaidi ya tano jukwaani,mbele ya wakazi wa mji huo ambao walishangilia na kupiga mayowe kila kona ya Uwanja.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Kayanga,Karagwe mjini asubuhi hii kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Misenyi asubuhi hi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wakazi wa mji wa Misenyi  katika viwanja vya mashujaa wakishangilia mara huku wakiendelea kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.

Waziri amchefua Magufuli

g4 


*Aomba Watanzania wamtetee kwa uamuzi atakaochukua

Na Bakari Kimwanga, Muleba
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameahidi kushughulika na mmoja wa mawaziri aliyegawa ranchi za mifugo kiholela.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana, alipohutubia mikutano ya kampeni iliyofanyika katika miji ya Muleba na Kamachumu mkoani Kagera.
Alisema hawezi kukubali kuona wananchi wanaendelea kuteseka wakati watu fulani wanamiliki ranchi hizo, huku migogoro isiyomalizika ikiendelea kufukuta.
Hata hivyo, katuika mkutano huo, Dk. Magufuli hakumtaja waziri huyo wala alikuwa katika serikali ya awamu gani, isipokuwa alisisitiza kupambana naye akiingia madarakani.
“Ninajua hapa kuna mgogoro wa ranchi ya Rutoro ambayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongela amesema anaushughulikia. Nawaambia mkoa wenu una ranchi 52 ambazo zimegawiwa kiajabuajabu.
“Hakuna jambo linalomuumiza kichwa Rais Kikwete, kama uamuzi huu wa mtu mmoja kugawa ovyoovyo maeneo haya kwa watu ambao hawana ng’ombe wala mbuzi…nasema hili hapana.
“Sitawaangusha, tutakwenda kupambana na watu hawa ambao wameharibu,” alisema Dk. Magufuli.
Alisema hayuko tayari kuona wananchi wanaumia kwa makosa yaliyofanywa na watu walioaminiwa katika utendaji serikalini.
“Kama mtanichagua kuwa rais, tutagawa baadhi ya maeneo na kuwapa wananchi ili wapate maeneo ya malisho ya mifugo na kilimo,” alisema Dk. Magufuli.

SOKO LA KAHAWA
Kuhusu soko la kahawa, mgombea huyo alisema anatambua changamoto zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Alisema anashangazwa na bei ya kahawa inayotoka Kagera kwenda Uganda kuwa na soko kubwa, wakati nchini bei imezidi kushuka kila kukicha.
“Ikulu ni ya Magufuli na CCM, wengine wasindikizaji. Msiwasikilize, ninaomba kura zenu zote Watanzania,” alisema.
Alisema anaomba urais kwa ajili ya kuwatumikia wananchi ambao wanaonekana kukatishwa tamaa na baadhi ya watendaji wa serikalini ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao.

AHADI YA MELI
Alisema ahadi iliyotolewa na Rais Kikwete kila ziwa kubwa kuwa na meli iko palepale.
Aliwaasa wananchi wa Kagera kuepuka kauli za wanasiasa kufanya ajenda ya meli kuwa mtaji wa kuombea kura.

TIBAIJUKA APIGA MAGOTI
Katika hatua nyingine, mgombea ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini kupitia CCM, Profesa Anna Tibaijuka, aliwavunja mbavu wananchi baada ya kuomba kura akiwa amepiga magoti.
Akiwa mbele ya Dk. Magufuli, Profesa Tibaijuka aliomba asaidiwe kupata barabara ya lami.
“Ninaomba nikipiga magoti kwako mgombea urais, pamoja na maendeleo mengine kupatikana, naomba barabara ya lami kuelekea Hospitali ya Rubya…yaani imekuwa kero wakati mvua zinapoanza kunyesha,” alisema Profesa Tibaijuka huku akishangiliwa.

AOMBA KUTETEWA
Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli, amewaomba Watanzania wamtetee kutokana na uamuzi atakaochukua dhidi ya viwanda vya umma visivyoendelezwa.
Alisema kutokana na uamuzi huo, watu wasiomtakia mema wageuza ajenda hiyo na kudai atawanyanyasa wafanyabiashara.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano aliofanya Jimbo la Bukoba Vijijini jana na kusema dhamira ya kuchukua viwanda visivyoendelezwa ipo palepale na hatorudi nyuma.
“Watanzia niteteeni kwa kunichagua kwa kura nyingi, niliposema tutachukua viwanda vilivyoshindwa kuendelezwa, kuna watu wanageuza maneno na kusema nitawaonea wauza maduka.
“Siwezi kufanya hivyo, wenye maduka wengi wao ni wanyonge ambao mimi ndiyo mtetezi wao wa kweli.
“Leo viwanda vyote walivyobinafsishiwa watu, wameshindwa kuviendeleza, vimegeuka maghala ya mbuzi… hapa Bukoba tulikuwa na kiwanda cha chai kimekufa, vijana wetu hawana ajira wanaishi maisha magumu.
“Najua ninasimama hapa nikizungumza mafisadi hawanipendi na ninawaomba wana Bukoba na Watanzania mniombee.
“Najua hata hapa Bukoba wapo, wamekuwa wakileta hela zao ili msinichague, hela zao kuleni na mnichague kwa wingi,” alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa.

MAUAJI
Dk. Magufuli alilaani mauaji ya watu kwa kukatwa makoromeo, huku akisema suala hilo ni lazima likome kwani haliendani na ubinadamu.
“Kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake, anatakiwa kulaani mauji ya aina hii. Leo mtu unatoka kupata lubisi unakutana na mtu anakukata koromeo, huu ni utamaduni gani ndugu zangu?” alihoji Dk. Magufuli.
Mtanzania

Saturday, 19 September 2015

Tujivunie Zanzibar


Zanzibar ni sehemu pekee katika Dunia! Hili linasemwa na UNESCO, Watalii na sisi sote tunalijua hili. Hapa ni sehemu tunayoishi na kufanya kazi kwa Amani, Usalama na Uaminifu. Kila mwaka maelfu ya watalii huja nchini mwetu! Tumebarikiwa kuwepo hapa. Tunatakiwa tuwe na matumaini na Familia zetu hivyo tunaweza kuifurahia Zanzibar kila siku.

Tunajivunia kufanya kazi na rasilimali bora za nchi yetu, Ni watu, Ni Wazanzibari! Tujivunie Zanzibar.

________________________________________
­_
Zanzibar is a unique part of the world! This is said by UNESCO, by tourists, and we all know it! This is the place where we live and work in peace, security and faith! Every year hundreds of thousands of tourists from around the globe enjoy being in our country! We are blessed to live here every day, every single day should bring more hope for us and our families so we could enjoy Zanzibar throughout the time!

We are proud to work for the best assets our country has: It's people, It's Zanzibaris ! Let’s be proud of Zanzibar!